25/02/2026
TAARIFA KWA MAFUNDI WOTE WA KUPAUWA NYUMBA
Mafundi wenzetu, tunawasalimu!
Sisi tunawajua vizuri β tunajua juhudi zenu, tunajua changamoto zenu, na tunajua jinsi kazi zenu zinavyohitaji vifaa bora ili nyumba ipauke vizuri na kwa ubora wa hali ya juu.
Tunapenda kuwajulisha kwamba sisi tunauza mbao aina zote, zilizoidhinishwa na serikali, zenye ubora wa hali ya juu na bei rafiki kwa mafundi na wateja wote.
Tunawaomba kitu kimoja tu β pale unapokuwa na mteja wako, au umeshawahi kununua mbao kwetu halafu mteja wako akamuunganisha rafiki yake aje achukue mbao, tafadhali usimshawishi boss akanunue sehemu nyingine kwa sababu ya masilahi binafsi.
Njoo tufanye biashara pamoja, kwa uwazi na ushirikiano.
Kumbuka:
π° Mafundi mna bei zenu za ndani β tunawajali, tunawathamini, na tunahakikisha hamtapoteza.
π€ Tunathamini ushirikiano wenu, na tunapenda kuona mafundi wananufaika pamoja nasi.
Tushirikiane β ukileta mteja, hata sisi tunakupa faida yako rasmi, bila usumbufu wala mchezo.
π Sisi ni wauzaji wa mbao bora kutoka Mafinga β zenye ubora, uhalali na bei nzuri.